... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Heri Yule Anaye …

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Petro 2:1 Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.

Listen to the radio broadcast of

Heri Yule Anaye …


Download audio file

Jinsi tunavyowatazama watu wengine ndivyo inavyopelekea namna tunavyowatendea mara nyingi. Sasa jinsi tunavyowatazama wakati mwingine haijengi. Kwa hiyo naomba niulize, je! ni lini uliwahi kutathmini mitazamo yako unayoitumia kuwatazama wengine?

Kuna mitazamo hasi inayotia wasiwasi katika mahusiano yetu na watu wengine. Wivu ni mojawapo, Undugu ni mwingine. Mtazamo wa mtu kutaka kupendwa na watu au kutaka vya kwake tu ndo vikubaliwe. Mitazamo hiyo ninapenda kuiita “lenzi” mbalimbali. Je!, ni kwa kiwango gani zinaweza kupotosha namna tunavyowatazama watu wengine?, Je!, Ni kwa kiwango gani zinatupelekea kutendea wengine visivyo? Kufokea na kuumiza watu, kutumia hila, kuwa na wivu, kusingizia watu? 

Ebu jaribu kukumbuka siku uliyowahi kumuumiza mtu mwingine vibaya hata kumtendea vibaya … hadi kwa sasa, unajuta kabisa ulivyowafanyia. Sasa jiulize, Ni ishu gani maishani mwangu na katika mitazamo yangu, ni “lenzi” gani iliyosababisha niwatendee kama nilivyofanya? 

Sasa, ukitafakari hayo, msikilize Mungu akiongoea nawe kuhusu uhusiano huo: 

1 Petro 2:1  Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote. 

Mungu Baba yetu, kama vile baba mzazi yeyote anataka watoto wake wapendane kama vile anavyowapenda na sisi pia. Kweli, ni ushuhuda mzuri sana wa upendo wake Mungu wakati sisi tunawapenda wanaotuzunguka tukitumia upendo ule ule.  Kama vile mtu mmoja alivyosema … 

Heri mtu yule aliyejifunza kustahi wengine na kushangilia badala ya kuwa na wivu, aliyejifunza kusifu bila kujipendekeza au kubembeleza, aliyejifunza kuongoza bila kutawala kwa werevu.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.