... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Imani Dhaifu, Inayoyumba-yumba Lakini Yenye Unyenyekevu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 17:5,6 Mitume wakamwambia Bwana, Tuongezee imani. Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng’oka, ukapandwe baharini,, nao ungewatii.

Listen to the radio broadcast of

Imani Dhaifu, Inayoyumba-yumba Lakini Yenye Unyenyekevu


Download audio file

Rafiki yangu mpendwa, aitwaye Lowell Wertz, amekuwa sasa mishionari barani Afrika zaidi ya miaka 40.  Jana nikulishirikisha changamoto yake ya kwanza wakati Mungu anataka awe na imani kubwa. Leo ninapenda kukwambia changamoto yake ya pili.

Hayo ndiyo aliyoniandikia yafuatayo kutoka kwenye makau makuu ya huduma yake nchini Tanzania: 

“Ilikuwa Disemba fulani ambapo huduma yetu ilikuwa na madeni mengi kuliko tulivyowahi kuwa nayo. Mindy [ambaye bila shaka ni mhasibu wao] aliniandikia email akisema, mahesabu ya pesa yanaandikwa kwa kalamu yenye wino mwekundu inayoashiria hesabu iliyo hasi yaani mbovu, na sasa imekuwa nyekundu sana [akiwa na maana kwamba, deni limezidi sana kuongezeka]. Nilikatishwa tamaa kwa sababu kulikuwa na wahitaji wengi waliokuwa wananisubiri niwasaidie wakati ule. Sasa wakati natoka nyumbani kwenda kukutana nao, mke wangu Claudia aliniambia, “Usitumie pesa ambazo hatuna.” Wakati naendesha gari kwenda pale nisipojua, Bwana aliongea nami moyoni mwangu na kusema – “Mimi nimekuitia kuwa mishionari wangu.  Endelea utimize wajibu wako.” Kwa imani tuliwasaidia pesa watu ambazo hatukuwa nazo.  Ujumbe uliofuata kutoka kwa Mindy ulikuwa wa ajabu.  Alisema, kuna kitu kisicho cha kawaida ambacho kimetokea.  Sanduku la posta lilijaa bahasha za zawadi kuliko iliyowahi kutokea!  Tulimaliza mwaka ule tukitumia kalamu yneywe wino mweusi kwenye hesabu zetu [yaani tulikuwa na salio la kutosha].  Kuishi kwa imani si kupumbazika, hapana; lakini ni kanuni inayohitajika kama mtu anataka kufanya mapenzi ya Mungu – yeye Mungu anatoa thawabu kwa wale wenye imani hata kama ni imani dhaifu, inayoyumba-yumba yenye unyenyekevu. 

Ni kweli kabisa!  Kama vile mwanatheolojia na mwalimu aitwaye Dokta Barry Chant aliwahi kusema hivi, tunapopiga hatua ya imani, Mungu naye atatuonekania.  Lakini usikubali tu walichokisema Lowell na Barry.  Wala usinikubali mimi tu.  Sikiliza alichokisema Yesu:

Luka 17:5,6  Mitume wakamwambia Bwana, Tuongezee imani.  Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng’oka, ukapandwe baharini,, nao ungewatii. 

mwamini Yesu.  Yeye huwapa thawabu wale wenye imani na unyenyekevu hata ikiwa dhaifu na ya kuyumbayumba. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.