... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kutoridhiana

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Tito 3:3-5 Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana. Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa; si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu.

Listen to the radio broadcast of

Kutoridhiana

Download audio file

Hakuna mkamilifu, Mimi sijakamilika wala wewe haujakamilika.  Hii inatuletea changamoto kama tumemwamini Yesu.  Kwasababu ahadi yake ni kwamba tukiweka tumaini letu kwake, atatupa maisha mapya.

Kwa upande mmoja, mtu akimwamini Yesu aliyekufa kwa ajili yake pale msalabani, dhambi zake zinasamehewa na kupitia ufufuko wake, anapewa maisha mapya. Lakini bado hofu, kushindwa, madhaifu na mapungufu vinaendelea kuwepo maishani mwa mtu. 

Kwanini Mungu asiingize mkono wake na kutukamilisha moja kwa moja?  kumbe kuna mchakato wa mabadiliko ambao huja hatua kwa hatua na kuna hatua za kuchukua. 

Tito 3:3-5  Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.  Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa; si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu. 

Sasa, mtu atafanyaje wakati bado kuna utengano kati ya theolojia na hali halisi kuhusu vipengele vya dhambi vinavyoendelea? Hivi karibuni nilimsikia mtu fulani akisema kwamba amejenga mtazamo kwa kutoridhika na mapungufu ya tabia zake za asili.  Ina maana kwamba, anafahamu vema kwamba amekuwa kiumbe kipya lakini pia ameelewa kwamba bado dhambi ipo.  Na hataki kuridhiana nazo. Hataki kuzikubali. Ataendelea kumruhusu Mungu “kumuosha” kila wakati kwa muda ameobakiza hapa duniani. 

Kutokuridhiana na mapungufu ya tabia zetu ni wazo zuri. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.