... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuwa na Moyo wa Uchunguzi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mithali 25:2,3 Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo; bali ni utukufu wa mfalme kuchunguza jambo. Mbingu huenda juu sana, na nchi huenda chini; lakini mioyo ya wafalme haichunguziki.

Listen to the radio broadcast of

Kuwa na Moyo wa Uchunguzi


Download audio file

Hivi, umewahi kujaribu kuondokana na hali ya kufuata utaratibu ule ule siku zote bila kubadili wala kufikiria? Wanasema kwamba alama za magurudumu ya magari katika tope ni kama kaburi ndefu, gari zinazofuata hazina budi kuzifuata madereva wapende, wasipende. Lakini hakika Mungu amekupa uwezo wa kutoka kwenye hali kama hiyo.

Kuna kitu kimoja  nimegundua pale nimepojikuta kwenye hali ya kujichosha nikirudia-rudia utaratibu uleule kana kwamba hakuna njia ya kutokea. Hali hiyo inasonga kabisa ubunifu wa mtu na kipaji chake cha kutunga vitu vipya – vyenye uwezo uliowekwa ndani ya asili ya kila mwanadamu na Mungu aliye Mbunifu na Muumba. 

Ukiwapenda au ukiwachukia, teknolojia ya kampuni ya Apple inajulikana kwa ubunifu wa pamoja na usanifu unaovutia. Na uwezo huo umewafanya tofauti kabisa na kampuni zingine, ukawafanya pia kuwa kwa muda fulani, kampuni tajiri kuliko zote duniani. Ubunifu huo na uwezo wa kutunga taratibu mpya umetokana kwa sehemu kubwa na Mbuni wao Mkuu wa miaka mingi aitwaye, Mheshimiwa Jonny Ive aliyewahi kusema hivi: 

Mimi naogopa sana hata kuchukia kuona watu hawana ubunifu hata kidogo wala hawataki kuchunguza lolote. Hii ni mizizi ya migogoro na vurugu katika jamii. 

Yaani hakukwepa kutamka wazi kabisa lakini maneno yake yana uhusiano na mada yetu ya leo, kwasababu moyo wa uchunguzi unaamsha ubunifu na utungaji katika fikra zetu.  Ni hatua ya kwanza kutoka kwenye hali ya kurudia-rudia utaratibu uleule siku zote. Lakini usiyakubali maneno yangu tu.  Ebu sikiliza anayoyasema Mungu pia kuhusu mada hii: 

Mithali 25:2,3  Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo; bali ni utukufu wa mfalme kuchunguza jambo.  Mbingu huenda juu sana , na nchi huenda chini; lakini mioyo ya wafalme haichunguziki. 

Ni kweli, Mungu huwa anaficha mambo mengi tu.  Lakini ni jambo la utukufu pale tulipoumbwa kwa sura yake kwa moyo wa uchunguzi na hatimaye kugundua yaliyofichika. Hii ni hatua yako ya kwanza kutoka kwenye hali ya kurudia-rudia utaratibu ule ule siku zote! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.