... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Makosa Wanaume Wanayofanya (1)

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Petro 3:7 Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.

Listen to the radio broadcast of

Makosa Wanaume Wanayofanya (1)


Download audio file

Kusema ukweli, wanamume mara nyingi wanakuwa wakali kwenye familia zao.  Sitanii!  Kwasababu moja ama nyingine, hatutafakari yale familia zetu zinahitaji kwetu, kwahiyo tunarudia-rudia makosa yale yale kila siku.

Kosa kubwa la kwanza wanaume wanalolifanya – na ni kosa ambalo ninakiri kwa huzuni kwamba nimelifanya mara nyingi – ni kutokuheshimu wake zao.  Mpango wa Mungu kwa ajili ya familia ni kwamba zijengwe kwenye msingi imara wa umoja wa kuhurumiana kati ya mume na mke.

Ule umoja huwa unavunjika kila wakati – wanaume mnisikilize kidogo – huwa tunakosa kuonyesha heshima.

1 Petro 3:7 Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.

Changamoto endelevu ya mume yoyote ni kumwelewa mke wake kabisa – nadhani ni kazi ya ugunduzi unaoweza kuchukua maisha yote ya mtu.  Baada ya kusema haya, sisi wanaume tumeagizwa kuishi na wake zetu kwa akili kwa sababu kusemna ukweli wako tofauti sana na jinsi tulivyo sisi.

Ni kweli kabisa kwamba hawana nguvu kama sisi, lakini ni katika hali hiyo ya udhaifu, ndipo Mungu anaagiza waume kuwaonyesha heshimu. Hakuna kutumia maneno makali. Hakuna kumdhalilisha mbele za watu wengine.  Hakuna nafasi kabisa ya kumpiga.  Hayo yote ni marufuku!

Na kwasababu Mungu yuko makini sana kuhusu utekelezaji wa agizo hilo, ndiyo sababu tusipomtii, yeye ataacha kusikiliza maombi yetu.

Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.