... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mkono wa Msaada

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mithali 3:27,28 Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda. Usimwambie jirani yako, Nenda, urudi halafu, na kesho nitakupa; nawe unacho kitu kile karibu nawe.

Listen to the radio broadcast of

Mkono wa Msaada


Download audio file

Je! Umewahi kumwona mtu maskini na mhitaji kabisa kisha ukajiuliza, Kwa nini watu wasimsaidie?Kwa nini asisaidiwe na serekali au kanisa au hata  mtu ye yote?

Nadhani sisi sote tumewahi kufikiri hivyo mara kwa mara.  Mfano, wakati tukamwona muomba-omba barabarani akinuka vibaya, au mtu mwenye kansa isiyotibika kama ya ubongo. Au binti aliyebebeshwa mimba na sasa anaumwa huku akijaribu kutafuta chakula kwa ajili ya watoto wake. Au yule ambaye unaketi karibu naye kanisani lakini ameshindwa kuendelea kulipa mkopo kwa ajili ya gari lake.  Kwa nini mtu asimsaidie? 

Lakini kumbe, kuna wazo ambalo labda litakushtua.  Je! Mtu unayemtaja kwamba labda angetoa msaada ni kwanini asiwe wewe mwenyewe? 

Mithali 3:27,28  Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda.  Usimwambie jirani yako, Nenda, urudi halafu, na kesho nitakupa; nawe unacho kitu kile karibu nawe. 

Ni kipi kinachomstahilisha mtu apewe msaada wako? Ni kwa kuwa ni binadamu, na kwa sababu ya udhaifu alio nao na kwamba ameumbwa kwa sura yake Mungu, Basi, Hakuna la ziada. 

Na mimi ninaelewa vizuri kwamba ni rahisi kuwapuuza kwasababu ni usumbufu, kwasababu uko bize sana, kwasababu … kuna sababu nyingi tu. 

Lakini kusema ukweli, ni fursa na baraka pia kama tunaweza kumsaidia mtu katika mahitaji yake.  Si kwamba lazima tutoe hela; hata neno la kuwatia moyo, maongezi mkichangia chai, kuwastahi, kuwaunga mkono kwa kazi ngumu.  Kwa sababu mkono wako unakuwa mkono wa Mungu kwa ajili ya mtu yule. 

Kama vile rafiki yangu mmoja aitwaye Toni Gattari alivyosema … Kutoa ni kuishi kweli kweli. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.