... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Si Kwasababu Tunastahili, Bali ni Kwa Rehema

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Warumi 11:32 Maana Mungu amewaunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote.

Listen to the radio broadcast of

Si Kwasababu Tunastahili, Bali ni Kwa Rehema


Download audio file

Baada ya siku chache tutasherehekea Krismasi, tukikumbuka namna Mungu alivyofanyika mmoja wetu, Yesu alizaliwa, ili atuokoe na dhambi zetu na hukumu ya milele tuliyostahili.  Lakini ni kwanini?  Kwanini ilimbidi afanye hivyo, ni kwa msingi gani?

Nataka kuuliza hivi, Kwanini Mungu hakutuumba na uwezo wa kumpenda, kumheshimu na kutenda haki, Siingekuwa rahisi sana?  Siingekuwa safi jamani? 

Halafu, waliochagua kutenda mema na kumheshimu wangeenda mbinguni … kama wanavyostahili. Na walioamua kuishi kinyume chake, wangeenda Jehanamu, na ingekuwa haki, si kweli?  Ni rahisi sana. 

Lakini kumbe; sisi hatuna uwezo wa kuchagua kuishi maisha mazuri, maisha makamilifu. Sote tunatenda dhambi. Ukijiangalia kwenye kioo utafikia maamuzi hayo. Kwanini basi, Mungu aliandaa iwe hivyo?  Sijui kama umewahi kujiuliza swali hilo?  Basi … acha nikwambie jibu. 

Warumi 11:32  Maana Mungu amewaunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote. 

Hapa tunapata jibu.  Mungu ndiye aliyepanga iwe hivyo. Ametuunga sote pamoja katika uasi.  Kwasababu gani?, ni ili aturehemu sote ili tuweze kutambua pendo lake jinsi lilivyo kubwa. 

Hakuna pendo kubwa kuliko kusamehe watu makosa yao. Hakuna pendo kubwa kuzidi kukubali kupokea hukumu ya waliokuumiza.  Hakuna upendo mkubwa kuzidi mtu kufa kwa ajili ya dhambi za wengine 

Maana Mungu amewaunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.