... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Tujaribu Tena

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Kutoka 34:6,7 BWANA akapita mbele yake, akatangaza, BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa huruma, wenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na nne.

Listen to the radio broadcast of

Tujaribu Tena

Download audio file

Tabia ya Mungu na asili yake kabisa jinsi alivyo kwelikweli, watu wanaweza kuielewa vibaya.  Kwasababu Mungu amejidhihirisha kama Mungu wa upendo, lakini pia Mungu wa hukumu; Mungu anayesamehe na Mungu anayeadhibu na hatimaye kulaani na kutuadhibu milele.

Ndio maana watu wamechanganyikiwa. Ndio maana watu wengine wanamdhihaki Mungu kwasababu ya tabia zake tofauti-tofauti zisizofnanana. 

Wakati Musa alipokuwa kwenye mlima wa Sinai akipokea mbao mbili zenye Amri Kumi za Mungu, watu wa Mungu pale chini walikuwa wanajitengenezea  sanamu – ndama ya dhahabu jamani! 

Mungu alighadhibika mno, akitaka kuwashushia msiba mkubwa.  Hata Musa alivunja mbao zile za kwanza lakini baadaye akamsihi Mungu asiwadhuru watu wake.  Kwahiyo Mungu alimwamuru Musa kupanda mlima mara ya pili … akipeleka mbao mbili zingine.  Wakati alifika kwenye kilele cha mlima … 

Kutoka 34:6,7  BWANA akapita mbele yake, akatangaza, BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa huruma, wenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na nne. 

Mungu ni Mungu wa haki.  Ndio, dhambi zetu zinamkasirisha. Lakini tukimgeukia, tukitubu, anatusamehe.  Amejaa upendo mwingi.  Anaweza kuaminiwa. Lakini kwa wao wasiomgeukia, wakikataa kutubu, basi … hawezi kusahau kuwaadhibu wenye hatia. 

Bwana ni Mungu wa fadhili na huruma. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.