... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Unatafutwa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 19:9,10 Yesu akamwambia, Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu. kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.

Listen to the radio broadcast of

Unatafutwa


Download audio file

Penda, usipende, sisi sote tunapenda kupiga mahesabu kichwani kwa siri.  Na daftari letu la hesabu lina pande mbili, Upande wa muamala na upande wa deni; mambo mema tuliyoyafanya na mabaya tuliyoyatenda.  Sasa, ndani ya kiini cha mioyo yetu, tunao uhakika kwamba Mungu anachunguza sana daftari lile.

Lakini haitupasa kufikiri hivyo, Mungu ni Mungu wa neema na rehema, Mungu wa upendo na msamaha. Lakini hata hivyo, dhana ya daftari la mahesabu bado linakaa kichwani na ni vigumu kulifuta kabisa, si kweli? 

Jamani, jana niliharibu mambo kabisa, kwa hiyo Mungu hataki tena kuongea na mimi.  Bora nibaki mbali naye kwa muda. 

Lakini siku baada ya siku, utengano ule unaongezeka.  Kidogo, kidogo, unakuwa kama korongo kubwa mno tena lenye kina kabisa hadi mtu hawezi kufikiria namna atakavyoweza kuivuka. 

Kusema ukweli, Yesu alikosolewa sana na viongozi wa dini zamani kwasababu alipenda kukaa na watu waliojulikana kuwa ni wenye dhambi kuliko wengine, kama vile mtoza ushuru Zakayo na wenzake, Hawa walikuwa watu wabaya sana, wakidhulumu Waisraeli wenzao katika kutoza ushuru wakishirikiana na wakoloni Warumi.  Lakini … 

Luka 19:9,10  Yesu akamwambia, Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu.  kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea. 

Alitaka kusema nini, Yesu?  Kwamba alikuja kutafuta watu kama Zakayo, yaani wabaya kuliko wengine. Alikuja kwa ajili ya watu kama wewe na mimi.  Alikuja akitutafuta ili atuokoe – akatoa hata uhai wake kwa ajili yetu.  Yesu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.