... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Alilipa Deni Langu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Petro 2:21-24 Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake. Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake. Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki. Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.

Listen to the radio broadcast of

Alilipa Deni Langu

Download audio file

Viwango vya riba huwa vinapanda na kushuka, kiwango kikiwa juu  inakuwa vigumu kwa waliochukua mkopo na wana madeni kuweza kulipa. Na ni huzuni kwasababu kuna wengine mwishowe wanamezwa na madeni na wanapoteza vyote walivyokuwa navyo.

Ninakuombea usifikie hatua mbaya kama hiyo, na ninashukuru kwamba hata mimi sijafirisika hivyo. Nimeshuhudia watu wakinyanganywa nyumba kwakushindwa kurejesha mkopo waliochukua benki, benki wakaishika  nyumba na kuiuza,  Yaani ni tukio linalovunja moyo kabisa. 

Lakini hata hivyo … mimi ninakiri kwamba nina deni kubwa mno ambalo nisingeweza kulilipa daima. Deni ninalozungumza ni dhambi zangu, Yale makosa yote tuliyoyafanya, hakuna jambo lolote tungeweza kufanya kulipa deni zetu,  na kwasababu kiwango alichokitaka Mungu ni utakatifu mkamilifu, basi tungemezwa na madeni yetu, ila… 

1 Petro 2:21-24  Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.  Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake.  Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.  Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa. 

Kama vile mtu fulani alivyowahi kusema, Yesu alikuja kulipa deni ambalo hakulichukua yeye kwasababu sisi tulikuwa na deni ambalo tulishindwa kulilipa. Kinachobaki kwetu, wewe na mimi, ni kumwamini na kuacha kuishi katika dhambi. 

Alilipa deni langu na lako, alikufa kifo changu na chako.   

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.

We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy

Receive the FRESH devotional daily.

Dive deeper into God’s Word and grow closer to Jesus.

I want to receive God's Word FRESH daily!