... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Familia Kamilifu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Warumi 5:3-8 Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi; na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini; na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi. Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema. Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.

Listen to the radio broadcast of

Familia Kamilifu

Download audio file

Bila shaka umewahi kuwaza mara kwa mara: “Laiti familia yangu ingetengamaa kama familia zingine!”  Najua umewahi kufikiri hivyo, kwa sababu bado tunaamini hadithi ile ya “familia iliyokamilika”.  Kusema ukweli, familia ya hivyo haipo, Ni hadithi tu kama vile tunavyoweza kudanganya-danganya watoto kwa habari za Baba Krismasi.

Nataka kukushikirisha Maandiko fulani leo ambayo kwa mtazamo wa haraka haraka hayana uhusiano na swala la familia yako, lakini hata hivyo yasikilize 

Warumi 5:3-8  Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi; na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini; na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi.  Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu.  Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema.  Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. 

Yesu alikufa kwa ajili yako na kwa ajili yangu wakati tulipokuwa ni wenye dhambi; tulipokuwa waasi na wenye kukosa adabu. Kwa tendo lile alituonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi jinsi ililivyo kubwa. 

Kwahiyo, kadiri shida za kifamilia zinavyozidi kuja na kupita, je! Utafuata mfano huo?  Je! Utaonyesha wanafamilia wako pendo unalowapenda kwa kuchukuliana nao, kwa kujitoa na kuwa na moyo mkuu kwa ajili yao?  Je!  Utayafanya? 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.