... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Je! Imani Yako Inazidi Kukua?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Wathesalonike1:1-3 Paulo, na Silawano, na Timotheo, kwa kanisa la Wathesalonike, lililo katika Mungu Baba yetu, na Bwana Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba, na kwa Yesu Kristo. Ndugu, imetupasa kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kama ilivyo wajibu, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa kila mtu kwenu kwa mwenzake umekuwa mwingi.

Listen to the radio broadcast of

Je! Imani Yako Inazidi Kukua?

Download audio file

Je!, Mtu anawezaje kujua kama imani yake kwa Mungu inazidi kukua?  Je!  Inarudi nyuma au inabaki pale pale, au inapiga hatua mbele?  Mtu atatumia kipimo gani ili aweze kujua hali ya imani yake? 

Mtume Paulo ndiye aliyeandika karibia nusu ya “vitabu” vya Agano Jipya.  Vinatujia hasa kama “nyaraka”, yaani barua kwa makanisa aliyoyaanzisha au makanisa aliyotamani kuyatembelea. 

Kwahiyo, daima barua hizo zinaanza na salam za upendo kama barua hii ya pili aliyoliandikwa kwa kanisa la Thesalonike, kaskazini mwa nchi inayojulikana leo kama Ugiriki. 

2 Wathesalonike1:1-3  Paulo, na Silawano, na Timotheo, kwa kanisa la Wathesalonike, lililo katika Mungu Baba yetu, na Bwana Yesu Kristo.  Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba, na kwa Yesu Kristo.  Ndugu, imetupasa kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kama ilivyo wajibu, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa kila mtu kwenu kwa mwenzake umekuwa mwingi. 

Tukisoma nyaraka hizi, ni rahisi kuruka salamu hizi za utangulizi, lakini ni hasara kwetu kwasababu mara nyingi zinakuwa na ukweli wenye nguvu; kama vile hapa Mtume Paulo anaunganisha ukuaji wa imani yao pamoja na ukuaji wa upendo wa kila mtu kwa mwenzake. 

Kupenda wakorofi na wanaotusumbua si jambo rahisi hata kidogo. Lakini kadiri tunavyojifunza kuwapenda, kwa mtazamo wetu, na maneno yetu na jinsi tunavyowatendea, ndivyo tutakavyozidi kudhihirisha kina cha imani yetu ndani ya Yesu. 

Upendo Kumbe ndicho kipimo au rula ya kupimia imani yetu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.