... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kipimo Sahihi cha Tabia ya Mtu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yeremia 17:7,8 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA, ambaye BWANA ni tumaini lake. Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, uenezao mizizi yake karibu na mto; hautaona hofu wakati wa hari ujapo, bali jani lake litakuwa bichi; wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, wala hautaacha kuzaa matunda.

Listen to the radio broadcast of

Kipimo Sahihi cha Tabia ya Mtu


Download audio file

Kuna wakati maisha pale mtu anapobanwa sana, mambo yakipamba moto kabisa. Wakati anajisikia kwamba kuna ukosefu wa maji ya uzima Yesu aliyoahidi. Sehemu kama hiyo, kumbe inaweza kutudhihirishia jinsi tulivyo kweli kweli!

Halijoto kali kuliko zote nilizowahi kuona ilikuwa mwaka 1977, ilikuwa kwenye siku  ambayo binamu yangu Ted anafunga ndoa. Halijoto ilifika kiwango cha nyuzi joto 48!, tulitoka kwenye gari zilizokuwa na AC na kuelekea kwenye kanisa, yaani tulitaabika kweli! Sijui kama mtu angeweza kuishi kwenye joto la namna hiyo? 

Hii ndio picha inayonijia kichwani siku niliyosoma mistari hii ifuatayo: 

Yeremia 17:7,8  Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA, ambaye BWANA ni tumaini lake.  Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, uenezao mizizi yake karibu na mto; hautaona hofu wakati wa hari ujapo, bali jani lake litakuwa bichi; wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, wala hautaacha kuzaa matunda. 

Kesho yake tulitembelea bustani kubwa ya machungwa ya wakwe zake Ted.  Halijoto haikufikia kiwango kama siku ya harusi yake, lakini hata hivyo joto lilikuwa kali. Lakini Miti yote ya machungwa iliyojaa matunda kabisa!

Rafiki yangu, hicho ndicho kipimo cha tabia ya mtu.  Ni mtihani kupima kina cha uhusiano tulio nao na Mungu.  Je!  Tunaweza kuzaa … Je!  Tunazaa matunda wakati wa halijoto kali? Jibu ni inategemeana na namna mizizi yetu ilivyoenezwa ndani ya maji ya uzima. 

 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA … hautaona hofu wakati wa hari ujapo, bali jani lake litakuwa bichi; wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, wala hautaacha kuzaa matunda.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.