... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ukristo wa Starehe

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Wakorintho 5:15 Tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao.

Listen to the radio broadcast of

Ukristo wa Starehe


Download audio file

Acha nithubutu kukwambia kwamba hakuna “Ukristo wa starehe”.  Yaani, “Ukristo” na “starehe” ni maneno mawili yasiyoendana.  Kama wewe unataka kuendelea shwari maishani mwako bila matatizo, nakwambia kwamba Ukristo utakushinda.

Kama maelezo yangu yanakusumbua, basi ni jambo jema kwasababu Ukristo haukuanzia kwenye starehe na anasa, ulianzia kwenye msalaba ule katili wa Kalvari, msalaba uliopakwa damu. 

Wakristo wa kale waliudhiwa bila huruma kwasababu walitangaza kwamba Yesu alifufuka.  Pia, waliouawa kwasababu ya ushuhuda wa Yesu katika karne hii moja iliyopita, ni wengi mnoo kuzidi idadi ya waliouawa katika karne kumi na tisa zlizotangulia. 

Tena isitoshe, mateso dhidi ya Wakristo yanaongezeka pote duniani.  Wala, starehe na anasa si hali Kristo aliyotuitia, kwa sababu … 

2 Wakorintho 5:15  Tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao. 

Sasa acha nikuulize swali. Je!, Unajisikia kama unavutwa na starehe ikukumbutie kwenye mikono yake mitamu?  Usiwe na wasiwasi.  Hata mimi ninavutwa naye.  Ndivyo tulivyo kwa asili, tunapenda starehe na anasa.  Lakini kama unamwamini Yesu aliyekufa kwa ajili yako, basi ujue hili:  Alikufa ili uache kuishi kwa ajili ya nafsi yako mwenyewe. 

Rafiki yangu, Yesu alikufa na kufufuka ili umwishiye yeye.  Ni ukweli unaosumbua lakini ujue kwamba amekuweka pale ulipo ili umtumikie kwa gharama yoyote. 

Kuna watu maishani mwako ambao Yesu anataka upendo wake uwafikie kupitia wewe na vipawa na vipaji vyako vya kipekee ili waokolewe, wasife bila Kristo. 

Usidanganyike.  Hakuna Ukristo wa starehe na anasa.  Hakuna kitu kama hicho.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.