... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kutathmini Upya Wale Unaokuwa na Urafiki Nao

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Wakorintho 6:14,15 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?

Listen to the radio broadcast of

Kutathmini Upya Wale Unaokuwa na Urafiki Nao


Download audio file

Haitakiwi imani yetu ndani ya Mungu, wewe na mimi, iwe kama mwezi unaopevuka na kupungua. Hapana.  Kusudi lake Mungu ni kukuza imani yetu na kuiimarisha kupitia milima na mabonde ya maisha, kwa manufaa yetu na kwa utukufu wake.

Jana tulianzisha mada fupi kuhusu namna yakuimarisha imani yako kwa kumjibu mtu anayepokea ujumbe huu kila siku. Wakati tunaanza, tuliongea habari ya mambo mawili yanayoweza kuzuia imani ndani yetu – mizigo tunayobeba kutoka kwenye maisha yetu na dhambi inayotuzinga na kutuangusha. 

Leo tunataka kuchunguza jambo la tatu linalozuia imani – ni wale tunaokuwa na urafiki nao. 

2 Wakorintho 6:14,15  Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi?  Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari?  Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? 

Ni dhairi kwamba daima tutakuwa tumezungukwa na watu wadiomwamini Yesu. Na ndivyo inavyotakiwa iwe. Tunapaswa kuangaza nuru ya upendo wake maishani mwao. Lakini angalia vizuri namna Mungu anavyosisitiza aina ya mahusian, anasema … Msifungiwe nira pamoja na wasioamini. 

Anachokisema hapa Mungu ni kwamba, kadiri tunafanya mahusiano yale kuwa ya karibu zaidi, kadiri tunaruhusu wale wasiomwamini Yesu kutushawishi, hata wale  wanaompinga hadharani, ndipo wema wetu utabadilishwa kuwa kama uovu wao. 

Je! Unataka imani yako ndani ya Mungu ikoje?, Basi, usiwaruhusu wasioamini kukuvuta kutoka kwa Yesu.  Kwa kweli swala hili linahusu wale wanaopenda kukaa nao muda wote. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.