... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mbwa Wanaobweka

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 2:1-5 Basi, ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu, sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima.

Listen to the radio broadcast of

Mbwa Wanaobweka


Download audio file

Ujumbe kwamba Yesu alikufa msalabani ili dhambi za ulimwengu, ziweze kusamehewa.

Kwa upande mmoja, kila mtu siku hizi ana simu janja mkononi.  Kwa upande mwingine, kuna habari ya zamani sana kuhusu Yesu  aliyekubali kutundikwa msalabani na inasemekana kwamba alifufuka tena.  Kama nilivyosema, inashtua. 

Lakini habari ya Yesu daima imewakwaza watu.  Kwa kweli, alikwaza watu.  Ndiyo maana walimsulubisha. Mtume Paulo alieleza hivi: 

1 Wakorintho 2:1-5  Basi, ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu, sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima.  Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa.  Nami nalikuwako kwenu katika hali ya udahifu na hofu na matetemeko mengi.  Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu, ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu. 

Ni kama Wakorintho hawakupendezwa sana na yale ambayo Paulo aliyokuwa anataka kuwaambia.  Lakini kama vile Charles Spurgeon aliwahi kusema:  Waache mbwa wabweke, ni asili yao.  Wewe endelea kumhubiri Kristo, naye amesulubiwa. 

Kuna wakati tunakuwa na hofu kuwaambia watu habari za Yesu.  Paulo alijisikia mdhaifu na akatetemeka kwa hofu.  Kuna wakati hatuna maneno yanayofaa wala hekima.  Lakini tukiwaambia watu ukweli unaoshangaza kuhusu msalaba, tunacho kitu kimoja kabisa. Kitu hicho ni uwezo wa Roho Mtakatifu. 

Rafiki yangu, endelea kuwaambia watu habari za Yesu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.