... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ulimwengu Uliopoteza Dira

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Isaya 40:22-25 Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanokaa ndani yake huwa kama panzi; yeye ndiye azitandazaye mbingu kama pazia na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa; ndiye awatanguaye wakuu, na kuwabatilisha waamuzi wa dunia.

Listen to the radio broadcast of

Ulimwengu Uliopoteza Dira


Download audio file

Leo hii, kuna watu karibia Billioni moja ambao hawapati chakula cha kutosha wakati watu Billioni mbili na nusu wamenenepa kupita kiasi.  Mwaka huu, nusu Triliyoni za dola za kimarekani zitatumika kununua dawa haramu za kulevya.  Katika watu millioni 140 watakaokufa mwaka huu, zaidi ya nusu yao watakufa.

Najua kwamba wewe na mimi hatuwezi kuleta mabadiliko makubwa katika ulimwengu huu.  Pia kuna wakati maisha yetu ni kama yamepoteza dira. 

 Juzi nilikuwa ninaongea na Bwana na Bibi fulani ambao mtoto wao wa kiume, akiwa mtu mzima, alikuwa amelazwa hospitalini kwa sababu ya tatizo lake la kutumia dawa za kulevya.  Wale wazazi wana upendo mwingi, ni wacha Mungu waliojitahidi kulea watoto wao vizuri … lakini hata hivi, imetokea hivyo. 

Kwa hiyo, wakati maisha yanaelekea kuharibika kabisa kwa kupoteza dira, kuna maneno yatupasa kuyakumbuka: 

Isaya 40:22-25  Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanokaa ndani yake huwa kama panzi; yeye ndiye azitandazaye mbingu kama pazia na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa; ndiye awatanguaye wakuu, na kuwabatilisha waamuzi wa dunia.  Naam, hawakupandwa; hawakutiwa katika ardhi kama mbegu; naam, shina lao halikutia mzizi katika ardhi; tena awapuzia tu, wakanyauka, upepo wa kisulisuli wawaondoa kama mabua makavu.  Mtanifananisha na nani, basi, nipate kuwa sawa naye?  Asema yeye aliye Mtakatifu. 

Kama vile A.W. Tozer aliyewahi kusema: “Hata kama mambo yanaonekana kwamba yanaelekea kuharibika kabisa, huko nyuma bado kuna Mungu ambaye hajasalimu amri wala hajajiudhuru kutoka kwenye mamlaka yake.”  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.