... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Na Tazama …

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Ruthu 2:4 Na tazama, Boazi akaja kutoka Bethlehemu kawaamkia wavunaji, akasema, BWANA akae nanyi. Nao wakamwitikia, BWANA na akubariki.

Listen to the radio broadcast of

Na Tazama …


Download audio file

Aliyeoa au aliyeolewa atakwambia kwamba kuna wakati mke au mme anafanya kitu ghafla ambacho mwenzie hakutazamia hata kidogo. Unakuta Ulidhani unamfahamu vizuri lakini kumbe!

Tena ni jambo jema, kwa sababu linavutia. Ukweli ni kwamba, huwezi kumjua mtu asilimia mia, hata kama umeishi naye miaka hamsini au zaidi.

Sasa tutumie mfano huo kwa mahusiano tuliyo nayo na Mungu.  Hata kama tuna shauku kubwa kumfahamu, yeye ni mkubwa mno – ana uwezo wote, yuko sehemu zote, hana mipaka, hazuiliwi na muda kama sisi tunatawaliwa na ratiba – kwa hiyo mwelekeo wake kutushangaza ni mkubwa kuliko awaye yote ambao tunafahamiana naye.

Kama ulishasoma kitabu cha Ruthu kwenye Agano la Kale, utakumbuka kwamba alifiwa na mmewe akiwa bado ana umri mdogo akiishi ugenini.  Lakini kwa kuwa alibaki mwaminifu kwa mama mkwe wake Naomi (naye alikuwa mjane pia) basi, bila yeye kujua, Mungu alikusudia kumbariki. 

Kwahiyo, Ruthu alikuwa anahangaika shambani wakati tajiri wa shamba lile anajitokeza. 

Ruthu 2:4  Na tazama, Boazi akaja kutoka Bethlehemu kawaamkia wavunaji, akasema, BWANA  akae nanyi.  Nao wakamwitikia, BWANA na akubariki. 

Sasa ukiendelea kufuatilia habari hiyo, utafahamu kwamba hatimaye, Ruthu aliolewa na Boazi na Ruth (akiwa mtaifa jamani!!) anaonekena mmoja wa akina mama watatu wanaotajwa katika orodha ya ukoo wa Yesu katika sura ya kwanza ya Mathayo. 

Lengo langu kwa kukwambia hayo ni lipi?  Usimbane Mungu kwa kujaribu kumwingiza ndani ya katoni.  Usiruhusu matazamio yako yanayomhusu yawe hasi kiasi ambacho uhusiano wenu uwe wa kawaida tu.  Kwasababu yeye anapenda kutuonekania ghafla bila kutazamisha. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.