... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Si Kujitupa Gizani

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 12:44-46 Naye Yesu akapaza sauti, akasema, Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi bali yeye aliyenipeleka. Naye anitazamaye mimi amtazama yeye aliyenipeleka. Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye asikae gizani.

Listen to the radio broadcast of

Si Kujitupa Gizani


Download audio file

Kwa yule aliye nje ya imani, anaweza kufikiri kwamba kuamini kwamba huyu Yesu ni Mwana wa Mungu ni hatari. Wengi wanafikiri swala zima la imani ni kama mtu kajitupa gizani bila kujua ataangukia wapi.  Wewe unaonaje?

Zamani niliwahi kufikiria kama nitajiunga na hawa “Wakristo”, kweli nilikuwa na mashaka.  Je! Yesu angeniomba nifanyeje?, Je! Angenituma mwisho wa dunia kuwa mishionari (dhana ambayo haikunipendeza hata)

Na wewe, kama umewahi kukubali kumfuata Yesu, bila shaka utakuwa umeshapitia vipindi vyenye giza hadi unajiuliza, “Ni nini kinachoendelea?  Hayo yote yana maana gani? Je! Kuna faida yoyote?” Maswali kama hayo yanakuja kwasababu ni sehemu ya kuishi kwa imani.  Unajua, kama ungefahamu hatima ya kila jambo, usingehitaji kuwa na imani. 

Lakini Yesu hakukusudia hata siku moja kutuacha gizani. La!  Bali alisema hivi:

Yohana 12:44-46  Naye Yesu akapaza sauti, akasema, Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi bali yeye aliyenipeleka.  Naye anitazamaye mimi amtazama yeye aliyenipeleka.  Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye asikae gizani. 

Alitamkaje?  Alipaza sauti! Alisemaje? Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye asikae gizani.  

Kumbe!, Imani ndani ya Yesu si kujitupa gizani, bali ni hatua ya kuingia Nuruni! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.